Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Prof Raphael Chibunda Awataka Watumishi Wa Kampasi Ya Mizengo Pinda Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano

Prof. Chibunda amewataka watumishi wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda kufanyakazi kwa ushirikiano ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika kampasi hiyo. Aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili katika Kampasi ya Mizengo Pinda Novemba 7 – 8, 2022.

Katika ziara hiyo, Prof. Chibunda alipokea ripoti ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kampasi hiyo na kupata fursa ya kutembelea miradi hiyo.

Pia, Prof. Chibunda aliongeza kusema kwamba kupitia serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuboresha sekta ya elimu ya juu nchini ikiwemo Kampasi ya Mizengo Pinda.  Kiasi cha pesa takribani bilioni ishirini zimetengwa kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza Kampasi ya Mizengo Pinda. Pesa hizo zinatarajiwa kutumika kujenga majengo matatu ambayo ni jengo la Taaluma linalokadiriwa kuchukua wanafunzi zaidi ya elfu mbili (2000) kwa wakati mmoja, maabara za kufundishia pamoja na dahalia.

Related Posts

Safari ya Mhitimu wa SUA Kuelekea Ujasiriamali wa Bidhaa Zitokanazo na Rasilimali  Nyuki

Katika picha, aliyeshika chupa za asali ni Dwasi Denis Johnson, mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Awali ya Usimamizi wa...

Kaimu Rasi wa Ndaki, Prof. Anna Sikira, Atoa Mwongozo kwa Wanachuo Wapya Kampasi ya Mizengo Pinda

Kaimu Rasi wa Ndaki, Prof. Anna Sikira, amewahimiza wanachuo wapya kujitambua na kufahamu kwamba lengo kuu la kuja katika Chuo...

Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) na Halmashauri ya Mpimbwe Yaingia Ubia wa Kielimu na Utafiti kwa Maendeleo ya Kilimo

Katika hatua ya kipekee ya kushirikiana kwa maendeleo ya jamii, Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)  kimeungana na Halmashauri...