Prof John Jeckoniah, Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) akiwasilisha mada ya masuala ya kijinsia kwa wafanyakazi na wawakilishi wa wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda
Mtaalamu wa masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Prof John Jeckoniah amesema kuwa malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wafanyakazi na wanafunzi juu ya masuala ya Jinsia katika maeneo yao ili kuondoa unyanyasaji na ukatili wa masuala ya kijinsia pamoja na ukatili wa kingono.
Prof Jeckoniah amesema kuwa kupitia mafunzo hayo na Uanzishwaji wa Kitengo na Dawati la Jinsia katika Chuo litasaidia kuondoa changamoto na matukio ya Unyanyasaji wa Kijinsia na kingono na matukio yaliyokuwa yakiripotiwa mara kwa mara kwenye Vyuo mbalimbali na Taasisi nyingine.
Pia Prof Jeckoniah amesema Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Tayari kimeandaa sera ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na muongozo wa uanzishwaji wa kitengo cha Jinsia na Dawati la Jinsia.
Mwisho Prof Jeckoniah Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema Elimu hiyo ili kusaidia Jamii kuondokana na Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika Jamii.