Hafra fupi ya kuwaapisha viongozi wapya wa Serikali ya wanafunzi kampasi ya Mizengo Pinda iliongozwa na Prof Anna Sikira (Naibu Rasi Taaluma Kampasi ya Mizengo Pinda).
Mara baada ya zoezi la kuwaapisha viongozi hao, Prof Sikira alipata wasaa wa kutoa nasaha fupi kwa viongozi wote waliokula kiapo cha uongozi, ambapo amewataka viongozi walioapishwa kuiongoza Serikali ya wanafunzi Kampasi ya Mizengo Pinda kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutimiza majukumu yao kama viongozi na kuongeza juhudi katika masomo ili kuwa mfano kwa wale wanaowaongoza.
Pia Prof Sikira amewataka viongozi hao pindi wanapokuwa na changamoto yoyote wasisite kufika ofisini kwake au ofisi ya mshauri wa wanafunzi ili kuweza kutatua changamoto hizo kwa pamoja na amewaahidi kushirikiana nao na kuzifanyia kazi changamoto zote zilizopo kwa ustawi wa Kampasi ya Mizengo Pinda.
Prof Anna Sikira (Naibu Rasi Taaluma Kampasi ya Mizengo Pinda), akitoa nasaha fupi kwa viongozi walioapishwa kuiongoza Serikali ya wanafunzi
Serikali ya wanafunzi itaongozwa na mwenyekiti aliyechaguliwa Ndugu Bulongo William Cosmas, akishirikiana na makamu mwenyekiti Bi Mshana Mary na Katibu wa Serikali ya wanafunzi Ndugu Mahewa Naftari.
Uongozi wa Serikali ya wanafunzi unaunda jumla ya Baraza ya kamisheni tano, ambazo ni Kamisheni ya Elimu na Mikopo, Kamisheni ya Katiba na Sheria, Kamisheni ya Afya na Asasi za Jamii na Makundi Maalum, Kamisheni ya Mambo ya Njee na Kamisheni ya Michezo,Habari na Burudani.
Katika picha ni baadhi ya viongozi wakila kiapo cha kuitumikia Serikali ya wanafunzi