Bodi ya Ukaguzi ya SUA Yafanya Ziara katika Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika jitihada za kuimarisha ubora wa elimu na utafiti, Bodi ya Ukaguzi ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) ilifanya ziara ya kikazi kwenye Kampasi ya Mizengo Pinda tarehe 13 Machi 2024. Ziara hii ilikuwa na lengo la kukagua maendeleo na shughuli mbalimbali zinazoendelea kampasini, ikiwa ni pamoja na miradi mipya ya maendeleo. Wajumbe Waliotembelea, Dkt. Charles Lyimo (Mwenyekiti),Arnold Mbwambo (Katibu Msaidizi),Tryphone Ngoja na Dismas Myinga.

Wajumbe walipokelewa kwa mikono miwili na timu ya Idara ya Manunuzi, wakiongozwa na Bwana Daudi Ally Fungo. Walipata fursa ya kutembele maeneo muhimu ya kampasi, ikiwemo kiwanda cha matofari, mashine ya kuchakatia asali, na chumba cha kompyuta kinachotumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kujifunzia kwa vitendo.

Ziara hii ilileta mwanga mpya kuhusu maendeleo ya kampasi, hasa katika kuendeleza elimu na uchumi wa kampasi. Vifaa vipya vilivyonunuliwa vinaashiria hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Kituo cha kutolea huduma za afya kilichokaguliwa kinaonesha dhamira ya SUA katika kuhakikisha afya bora kwa wanafunzi na wafanyakazi.

Kampasi ya Mizengo Pinda, ikiwa ni sehemu ya SUA, inaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kukuza elimu na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii. Bodi ya Ukaguzi imejionea na kuridhika na maendeleo yaliyopo, na ina imani kuwa kampasi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Related Posts

Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo...

🌟 A CALL FOR SEMINAR 🌟

We are delighted to invite all students to a mandatory seminar to provide valuable insights and guidance on key aspects...