Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwanamvua Hoza Mrindo, na wageni mbalimbali walioudhuria sherehe hizo katika hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa majengo mapya ya Kampasi ya Mizengo Pinda na Kampuni ya TIL CONSTRUCTION. Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 17.5 za Kitanzania.

Kupitia mradi huu, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kitajenga jumla ya majengo 9, ambapo majengo mawili yatajengwa katika Kampasi ya Solomon Mahlangu, majengo matano yatajengwa katika Kampasi ya Edward Moringe, na hapa Kampasi ya Mizengo Pinda yatajengwa majengo mawili.

Jengo la taaluma litakuwa na eneo la mita za mraba 5,840 na litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja, na jengo la pili ni hosteli yenye ukubwa wa mita za mraba 5,132 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati mmoja.

Mbali na majengo hayo, utajengwa mfumo wa maji taka pamoja na jengo litakalokuwa na vifaa vya kuzalishia, kuhifadhi, na kusambaza umeme, ikiwa ni pamoja na jenereta zinazotumika wakati wa dharura.

Prof. Raphael Chibunda amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake binafsi za serikali ya awamu ya sita katika kuwezesha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa mradi wa kuendeleza sekta ya elimu ya juu nchini na kwa kuendelea kukiwezesha chuo kulipia gharama muhimu za uendeshaji wa chuo.

Vile vile, Prof. Chibunda ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa na Mh. Adolf Faustine Mkenda (MB), Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Omary Juma Kipanga (MB), na Prof. Crolyne Ignatus Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na viongozi wengine wote wa wizara kwa misaada na miongozo wanayoipatia chuo na kukiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, na mwakilishi wa Kampuni ya TIL CONSTRUCTION wakisaini mkataba wa ujenzi wa majengo mapya ya Kampasi ya Mizengo Pinda. Hafla hiyo ilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.

Related Posts

🌟 A CALL FOR SEMINAR 🌟

We are delighted to invite all students to a mandatory seminar to provide valuable insights and guidance on key aspects...

Michezo Huimarisha Afya

Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Kampasi Ya Mizengo Pinda mbali na kufundisha, kufanya tafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu...