Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Techknolojia, Mh. Omary Juma Kipanga akiteta jambo na mwenyeji wake Rasi wa Ndaki ya Mizengo Pinda, Prof Josiah Katani na mkuu wa wilaya ya Mlele Mh Sanga pindi alipotembelea katika kampasi hiyo.
Wakati huohuo Mh. Kipanga alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa SUA, Viongozi wa halmashauri ya Mlele pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya.
Mh. Kipanga amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuboresha sekta ya Elimu na katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua Kampasi ya Mizengo Pinda imetengewa kiasi cha shilingi Billioni ishirini kwaajili ya ujenzi wa majengo matatu, Jengo la Taaluma, Jengo la Mabweni na Jengo la Daharia.
Pia, Mh. Kipanga amemtaka Rasi wa Ndaki Prof. Josiah Katani kusimamia vyema fedha inayotolewa na Mh. Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania iendane na thamani ya majengo yatakayojengwa kwa maendeleo ya sekta ya Elimu na Nchi kiujumla.