Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Kampasi Ya Mizengo Pinda mbali na kufundisha, kufanya tafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu na uzalishaji mali katika nyanja za kilimo, mifugo, maliasili na utalii, pia watumishi na wanachuo ushiriki katika mambo mbalimbali ya kijamii kama kuchangia damu,michezo.
Katika Picha: Baadhi ya wachezaji wa timu ya watumishi wa Kampasi ya Mizengo walipokwenda kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Idara ya Afya ya Halmashauri ya Mpimbwe. Mchezo huo uliochezwa katika kata ya Mamba, Halmashauri ya Mpimbwe, ulihusisha michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa pete, draft, bao, na mpira wa wavu.
Katika Picha ni Timu ya Watumishi wa Idara Afya ya Halmashauri ya Mpimbwe.
Picha ya pamoja
Mchezo wa draft ulionesha ujuzi wa Prof. Makinda, Naibu Kaimu Rasi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Kampasi ya Mizengo Pinda, na Dkt. Herman Osca Ntungwa wa Kampasi ya Mizengo Pinda, wakati walipocheza katika kata ya Mamba.
Mchezo wa bao pia ulishindanishwa, ukiwakutanisha watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Mhadhiri Msaidizi Mr. Yahaya na Mr. Godwine Tuloline Mwanzembe.
Katika picha: Dkt. Farida Kweka akionesha umahiri wake katika mchezo wa mpira wa pete wakati walipocheza dhidi ya watumishi wa Idara ya Afya wa Halmashauri ya Mpimbwe katika kata ya Mamba, kama sehemu ya kudumisha afya na kuimarisha ujirani mwema.