Mkurugenzi Mkuu Wa Minjingu Mines Fertilizer Ltd Dr. Mshindo Msolla atembelea Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda

Dr. Mshindo Msolla alipata nafasi hiyo ya kutembelea Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda wakati ya ziara yake ya kuwaendeleza wakulima wa nyanda za juu kusini kwa kuwaelimisha matumizi bora ya mbolea katika mazao.

Rasi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani akiwa  na mgeni wake Dr. Mshindo Msolla  Mkurugenzi wa Kampuni ya Minjingu Mines Ltd.

Kampuni ya Minjingu Mines Ltd inajishughulisha na uchimbaji, uchakataji na uzalishaji wa mbolea, pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani wa mbolea na kutoa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea katika mazao kama vile mahindi, mikunde, nafaka, mazao ya mizizi, mboga na viungo, mazao ya nyuzi, matunda na tumbaku.

Dr Mshindo Msolla ni mwanafunzi muhitimu wa Chuo kikuu cha sokoine cha Kilimo (SUA) katika falisafa ya uzamivu wa udongo, pia amewahi kuwa kocha wa timu ya mpira wa miguu ya Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Mwenyekiti mstafu wa klabu ya Yanga Africa.

Naibu Rasi wa Ndaki Mipango, Utawala na Fedha Prof. Jeremia Makindara akisalimiana na Dr. Mshindo Msolla.

Related Posts

Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) na Halmashauri ya Mpimbwe Yaingia Ubia wa Kielimu na Utafiti kwa Maendeleo ya Kilimo

Katika hatua ya kipekee ya kushirikiana kwa maendeleo ya jamii, Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)  kimeungana na Halmashauri...

Uteuzi wa Prof. Jeremia R. Makindara kuwa Kaimu Naibu Rasi wa Ndaki ya Kampasi ya Mizengo Pinda

Uteuzi wa Prof. Jeremia R. Makindara kuwa Kaimu Naibu Rasi wa Ndaki ya Kampasi ya Mizengo Pinda (Utawala na Fedha)