Katika banda hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipata nafasi ya kuona na kupata maelezo juu ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Chuo ikiwemo mafuta ya alizeti na asali na mara baada ya kupatiwa maelezo juu ya bidhaa hizo, Mhe. Mrindoko alizawadiwa mafuta ya alizeti.
Mhe. Mwanamvua Mrindoko akipokea zawadi ya mafuta ya alizeti kutoka Kwa mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda ndugu Evaristus Magani
Mhe. Mwanamvua Mrindoko aliambatana na mwenyeji wake Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mhe. Rodrick Mpogolo ambaye naye alikabidhiwa zawadi ya asali inayozalishwa na Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda.
Mhe. Rodrick Mpogolo akipokea zawadi ya asali kutoka Kwa Afisa udahili wa Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda ndugu Abel Magembe Lugimba
Wananchi nao wanaendelea kujitokeza kujifunza na kujionea bidhaa mbalimbali zitokanazo na rasilimali nyuki na kilimo katika maonesho hayo ambayo kilele chake ni tarehe 08- 08- 2023.
Wananchi mbalimbali wakiendelea kujifunza na kujionea bidhaa mbalimbali zitokanazo na rasilimali nyuki na kilimo katika banda la chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda