Katika zoezi hilo, Prof. Katani aliambatana na Naibu Rasi wa Ndaki Mipango, Utawala na Fedha Prof. Jeremia Makindara, Bwana Shamba wa Kamapasi ya Mizengo Pinda ndugu Tambalu Alphonsi pamoja na Mhadhiri Msaidizi katika fani ya Misitu ndugu Evaristus Magani.
Ukaguzi huo ulilenga kuangalia namna bora ya uboreshwaji wa uwekaji wa mabango ya makatazo ya uingizwaji wa mifugo katika eneo la Shamba la mafunzo unaofanywa na wakulima wanaolizunguka eneo hilo.
Rasi wa kampasi ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Usalama Kampasi ya Mizengo Pinda ndugu David Kayombo alipotembelea katika shamba la mafunzo ya chuo hicho lilipo Vilolo Mkoani Katani.