Kaimu Rasi wa Ndaki, Prof. Anna Sikira, amewahimiza wanachuo wapya kujitambua na kufahamu kwamba lengo kuu la kuja katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ni kusoma. Alisisitiza umuhimu wa kujituma katika masomo na kushirikiana ili kufanikisha malengo yao ya kitaaluma wakati wa semina ya ukaribisho
Kaimu Rasi wa Ndaki (Prof. Sikira) akitoa mwongozo kwa wanachuo wapya Kampasi ya Mizengo Pinda
Prof. Sikira pia aliwakumbusha wanachuo kulipa ada kwa wakati ili kuepuka usumbufu wakati wa mitihani. Aliongeza kuwa, wanachuo wanapaswa kutumia vyema ofisi za mshauri wa wanafunzi na ofisi nyinginezo za ndani ya chuo kwa ajili ya kupata msaada pale wanapokumbana na changamoto
Baadhi ya washiriki wa semina ya ukaribisho wa wanafunzi wapya
Katika mapokezi ya wanachuo wa mwaka wa kwanza, walikumbushwa umuhimu wa kuishi katika imani zao na kutenda matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu. Imam wa Msikiti wa Kibaoni, Shekhe Mwita Omari Salumu kutoka BAKWATA, pamoja na Frateri Augustine Mnyere kutoka TEC Parokia ya Usevya iliyopo kata ya Usevya, Halmashauri ya Mpimbwe, walitoa nasaha hizo kwa wanachuo.
Aidha, katika ukaribisho huo, vyombo mbalimbali na taasisi mbalimbali kama Takukuru, Bima ya Afya Taifa (NHIF), Uhamiaji, Polisi, na Dawati la Jinsia pia zilipata fursa ya kuzungumza na wanachuo wa mwaka wa kwanza
Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na baadhi ya wanachuo wa mwaka wa kwanza katika picha ya pamoja.