Safari ya Mhitimu wa SUA Kuelekea Ujasiriamali wa Bidhaa Zitokanazo na Rasilimali  Nyuki

Katika picha, aliyeshika chupa za asali ni Dwasi Denis Johnson, mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Awali ya Usimamizi wa Rasilimali Nyuki. Anatumia ujasiriamali wa bidhaa zitokanazo na rasilimali nyuki, kama asali ya nyuki wakubwa na wadogo, katika maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Katavi. Maonesho haya yana lengo la kuwakutanisha wajasiriamali, taasisi, wakulima, wafugaji na kutangaza utalii na fursa zote zipatikanazo katika mkoa wa Katavi.

Bw. Dwasi amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe, Bi. Shamimu Mwariko, kwa kuendelea kuwapa ushirikiano kama wajasiriamali wa Halmashauri ya Mpimbwe.

Kwa sasa, Bw. Dwasi ana mizinga ishirini (20) iliyopo kwenye kijiji cha Kanindi, yenye uwezo wa kutoa lita 15 hadi 20 za asali. Hivyo, Bw. Dwasi anawaomba wadau ambao wanaweza kumsaidia kupata mizinga ya kisasa inayogharimu kiasi cha shilingi milioni mbili (2,000,000) ili aweze kuzalisha zaidi asali.

Katika picha: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rungwa wakipata elimu kuhusu uzalishaji wa asali kupitia mdudu nyuki na kalenda sahihi ya uandaaji wa mizinga. Elimu hii ilitolewa walipotembelea banda la Halmashauri ya Mpimbwe katika Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi.

Related Posts

Former Prime Minister Mizengo Pinda Visits Mizengo Pinda Campus to Observe Development Activities

The Mizengo Pinda Campus of Sokoine University of Agriculture (SUA) in Katavi recently hosted an esteemed visitor, Hon. Mizengo Pinda,...

Learning Through Practice: SUA Students Visit Weather Station

At the Sokoine University of Agriculture (SUA) Mizengo Pinda Campus, the focus on experiential learning continues to set students apart...

SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yasheherekea Miaka 63 ya Uhuru Katika Mdahalo Ulioandaliwa na Halmashauri ya Mpimbwe

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Joseph Oswald Ruboha, akitoa mada ya...