SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yasheherekea Miaka 63 ya Uhuru Katika Mdahalo Ulioandaliwa na Halmashauri ya Mpimbwe

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Joseph Oswald Ruboha, akitoa mada ya mafanikio ya elimu na kilimo ndani ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania iliyobeba kauli mbiu “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu”.

Katika mdahaloKuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kama vile mahindi, mpunga, ngano, kahawa, chai, pamba, korosho, tumbaku, na sukari, ni moja ya mafanikio makubwa. Kwa mfano, uzalishaji wa mazao ya chakula kama mahindi, mpunga, na mtama umeongezeka maradufu kutoka tani milioni 5.6 mwaka 1961 hadi tani milioni 13.3 mwaka 2020. Aidha, uzalishaji wa mazao ya biashara kama pamba, kahawa, na chai umeongezeka kutoka tani 0.4 mwaka 1961 hadi tani 1.5 mwaka 2020.

Vile vile, kumekuwa na ongezeko la uwekezaji na ubunifu katika kilimo, ikijumuisha matumizi ya mbolea, mbegu bora, zana za kisasa, umwagiliaji, usindikaji na uhifadhi wa mazao. Kwa mfano, matumizi ya mbolea yaliongezeka kutoka kilo 3.7 kwa hekta mwaka 2002 hadi kilo 20.1 kwa hekta mwaka 2018.

Pia, ushiriki wa wanawake na vijana katika kilimo umekuwa mkubwa zaidi, ambapo wanawake sasa wanamiliki ardhi, kushiriki katika maamuzi, kupata mikopo na elimu ya kilimo. Kwa mfano, asilimia 76 ya wanawake wanaofanya kazi nchini Tanzania wanajihusisha na kilimo, ikilinganishwa na asilimia 68 ya wanaume.

Serikali pia imeanzisha sera mbalimbali za kilimo ambazo zimefanikiwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara, hivyo kuchangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa. Mfano wa sera na mikakati iliyopo sasa ni pamoja na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II), ambayo inalenga kuongeza ukuaji na tija ya kilimo, kupambana na umasikini, na kusaidia kupunguza madhara katika matumizi ya rasilimali na kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Programu nyingine ni pamoja na Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (“Building a Better Tomorrow, BBT”), ambayo imelenga kuongeza uzalishaji kupitia kuhamasisha vijana kushiriki kwenye shughuli za kilimo ili kufikia lengo la kutokomeza njaa na umasikini.

Kwa kuongeza, ruzuku na huduma za ugani zimelenga kumuinua mkulima, hata yule mwenye mtaji mdogo, kupata pembejeo kwa bei nafuu na elimu bure kuhusu uzalishaji wa mazao. Hii imeongeza tija na motisha kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao husika. Mikopo yenye riba ya chini (6-8%) pia inatolewa kwa wakulima, kuwawezesha kuwa na mtaji na kuwaondolea mzigo wa marejesho ya mikopo hiyo.

Ndg. Joseph Ruboha akisalimiana na Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Geofrey Pinda, alipowasili katika mdahalo wa sherehe ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika katika bwalo la chakula la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda iliyopo mkoani Katavi. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, Wanachuo wa SUA Kampasi ya Mizengo Pinda  na wananchi wa Wilaya ya Mlele.

Related Posts

Learning Through Practice: SUA Students Visit Weather Station

At the Sokoine University of Agriculture (SUA) Mizengo Pinda Campus, the focus on experiential learning continues to set students apart...

Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo...