Tatizo la Mawasiliano ya simu na Mtandao wa Intaneti katika Kampasi ya Mizengo Pinda na kata ya Kibaoni Mkoani Katavi kwa ujumla kupatiwa ufumbuzi

Suala hilo limewekwa wazi na Mh Nape Nnauye, Mbunge na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati akitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kwake katika taarifa fupi ya kampasi ya Mizengo Pinda iliyowasilishwa kwake na Rasi wa Kampasi Prof Josia Katani.

Rasi wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Prof. Josiah Katani akitoa taarifa fupi ya kampasi mbele ya Mh Nape Nnauye, Mbunge na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa ziara yake fupi katika Kampasi ya Mizengo Pinda 

Rasi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo, Prof Josiah Katani amemuomba Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye mambo makuu matatu,wakati wa kusoma taarifa fupi ya Kampasi kwa mheshimiwa Waziri, ambapo aliomba kufungiwa mtandao wa TTCL na Tigo ili kurahisisha mawasiliano Chuoni  na pili amemuomba mheshimiwa waziri kuunganishwa kwenye mkongo wa mawasialiano wa Taifa, na mwisho Prof katani amemuomba mheshimiwa waziri wa habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari kupatikana kwa masafa ya Redio mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kutumika katika kukitangaza Chuo.

Mh Nape Nnauye, Mbunge na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kwake katika taarifa fupi ya kampasi ya Mizengo Pinda iliyowasilishwa kwake na Rasi wa Kampsi Prof Josia Katani.

Mheshimiwa Nape Nnauye waziri habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ameipongeza menejimenti ya Chuo kwa ujumla kwa uanzishwaji wa Chuo hiki kimkakati chenye kusaidia nyanda za juu kusini na kozi zitolewazo katika Kampasi hii.

Mheshimiwa Nape amesema tayari Serikali ipo kwenye mpango wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  kufika hadi katika Kampasi na amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL kulifanyia kazi jambo hilo haraka iwezekanavyo.

Pili mheshimiwa Nape amesema amekuja Mkoa wa Katavi  kufungua masafa ya redio ya TBC Inyonga iliyopo Halmashauri ya Mlele Mkoani Katavi, ambapo kupitia redio hiyo itasaidia kuongeza mawasiliano katika mkoa wa Katavi na kuwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Mlele kufungua redio ya Jamii ili kufikisha taarifa kwa jamii.

Pia Mheshimiwa Nape amesema TTCL wanatarajia kuja kuweka mnara wa simu katika Kampasi ya Mizengo Pinda ili kuboresha mawasiliano, na aliweka wazi kuwa kuna jitihada zinaendelea ili kuwezesha  makampuni ya simu kama Tigo, Voda, Halotel na Airtel kushirikiana ili kuboresha huduma za mawasiliano na kufanya mawasiliano kuwa rahisi na bora zaidi.

Mheshimiwa Nape aliwashukuru wananchi wa kata ya kibaoni, wanafunzi na menejimenti ya Chuo kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kuwaomba wazidi kumuombea Afya njema na Maono aliyokuwa nayo Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani katika jitihada ya kuwaletea maendeleo wa Tanzania.

Picha ya pamoja kati ya Mh Nape Nnauye, Mbunge na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda

Picha ya pamoja kati ya Mh Nape Nnauye, Mbunge na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Viongozi wa Kampasi ya Mizengo Pinda na wawakilishi wa wanafunzi wa Kampasi

Related Posts

Learning Through Practice: SUA Students Visit Weather Station

At the Sokoine University of Agriculture (SUA) Mizengo Pinda Campus, the focus on experiential learning continues to set students apart...

SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yasheherekea Miaka 63 ya Uhuru Katika Mdahalo Ulioandaliwa na Halmashauri ya Mpimbwe

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Joseph Oswald Ruboha, akitoa mada ya...

Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo...