Viongozi wapya wa Serikali ya wanafunzi kampasi ya Mizengo Pinda wala kiapo cha kuitumikia Serikali ya wanafunzi kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao

Hafra fupi ya kuwaapisha viongozi wapya wa Serikali ya wanafunzi kampasi ya Mizengo Pinda iliongozwa na Prof Anna Sikira (Naibu Rasi Taaluma Kampasi ya Mizengo Pinda).

Mara baada ya zoezi la kuwaapisha viongozi hao, Prof Sikira alipata wasaa wa kutoa nasaha fupi kwa viongozi wote waliokula kiapo cha uongozi, ambapo amewataka viongozi walioapishwa  kuiongoza Serikali ya wanafunzi Kampasi ya Mizengo Pinda kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutimiza majukumu yao kama viongozi na kuongeza juhudi katika masomo ili kuwa mfano kwa wale wanaowaongoza.

Pia Prof Sikira amewataka viongozi hao pindi wanapokuwa na changamoto yoyote wasisite kufika ofisini kwake au ofisi ya mshauri wa wanafunzi ili kuweza kutatua changamoto hizo kwa pamoja  na amewaahidi  kushirikiana nao na kuzifanyia kazi changamoto zote zilizopo kwa ustawi wa Kampasi ya Mizengo Pinda.

Prof Anna Sikira (Naibu Rasi Taaluma Kampasi ya Mizengo Pinda), akitoa nasaha fupi kwa viongozi walioapishwa kuiongoza Serikali ya wanafunzi

Serikali ya wanafunzi itaongozwa na mwenyekiti aliyechaguliwa Ndugu Bulongo William Cosmas, akishirikiana na  makamu mwenyekiti Bi Mshana Mary na Katibu wa Serikali ya wanafunzi Ndugu Mahewa Naftari.

Uongozi wa Serikali ya wanafunzi unaunda jumla ya Baraza ya kamisheni tano, ambazo ni Kamisheni ya Elimu na Mikopo, Kamisheni ya Katiba na Sheria, Kamisheni ya Afya na Asasi za Jamii na Makundi Maalum, Kamisheni ya Mambo ya Njee na Kamisheni ya Michezo,Habari na Burudani.

Katika picha ni baadhi ya viongozi wakila kiapo cha kuitumikia Serikali ya wanafunzi 

Related Posts

Learning Through Practice: SUA Students Visit Weather Station

At the Sokoine University of Agriculture (SUA) Mizengo Pinda Campus, the focus on experiential learning continues to set students apart...

SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yasheherekea Miaka 63 ya Uhuru Katika Mdahalo Ulioandaliwa na Halmashauri ya Mpimbwe

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Joseph Oswald Ruboha, akitoa mada ya...

Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo...