Watumishi na Wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda wajengewa uwezo wa namna ya kuwatambua watu wenye mahitaji maalum na namna ya kuwahudumia

Semina iliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuwatambua watu wenye mahitaji maalum na namna ya kuwahudumia katika kufanikisha utoaji wa elimu jumuishi iliendeshwa na wataalamu mbalimbali wakiongozwa na Dr Thabita Lupesa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Katika semina hiyo mada mbalimbali ziliwasilishwa. Mada hizo ni pamoja na umuhimu wa elimu jumuishi, njia za kubaini watu wenye mahitaji maalumu na utoaji wa afua stahiki kwa watu wenye mahitaji maalum.

Katika semina hiyo pia,watumishi na wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda walipata nafasi ya kupima uoni wa macho na usikivu wa masikio.

Dr Thabita Lupesa  Mkuu wa Kitengo cha Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo akitoa mada juu ya masuala mbalimbali kuhusu elimu jumuishi

Ndugu Benigno Kumpanga mtaalamu wa masuala ya Elimu Jumuishi na mahitaji maaalum akitoa mada juu ya elimu jumuishi na namna ya kuwatambua watu wenye mahitaji maaalum

Ndugu Benigno Kumpanga akiwaongoza watumishi katika zoezi la kuchangamsha na kuuweka mwili sawa wakati wa semina

Related Posts

Jinsi Mradi wa Elimu ya Juu kwa  Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unavyochochea Maendeleo ya SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika picha mwenye tai nyekundu: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, akitoa maelezo...

🌟 A CALL FOR SEMINAR 🌟

We are delighted to invite all students to a mandatory seminar to provide valuable insights and guidance on key aspects...